Ezekieli 26:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sasa visiwa vitatetemeka katika siku ya kuanguka kwako; naam, visiwa vilivyo katika bahari vitafadhaika, kwa sababu ya kuondoka kwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa watu wa bara wanatetemeka kwa sababu ya kuanguka kwake; wakazi wa pwani, wametishika kwa kutoweka kwako! Biblia Habari Njema - BHND Sasa watu wa bara wanatetemeka kwa sababu ya kuanguka kwake; wakazi wa pwani, wametishika kwa kutoweka kwako! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa watu wa bara wanatetemeka kwa sababu ya kuanguka kwake; wakazi wa pwani, wametishika kwa kutoweka kwako! Neno: Bibilia Takatifu Sasa nchi za pwani zinatetemeka katika siku ya anguko lako; visiwa vilivyomo baharini vinaogopa kwa kuporomoka kwako.’ Neno: Maandiko Matakatifu Sasa nchi za pwani zinatetemeka katika siku ya anguko lako; visiwa vilivyomo baharini vinaogopa kwa kuporomoka kwako.’ BIBLIA KISWAHILI Sasa visiwa vitatetemeka katika siku ya kuanguka kwako; naam, visiwa vilivyo katika bahari vitafadhaika, kwa sababu ya kuondoka kwako. |
Nchi yatetemeka kwa sauti ya kuanguka kwao; Kuna kilio, sauti yake yasikiwa katika Bahari ya Shamu.
Kwa kishindo cha kutwaliwa Babeli nchi itatetemeka, Na kilio chake chasikiwa katika mataifa.
Bwana MUNGU amwambia Tiro neno hili; Je! Visiwa havitatikisika kwa mshindo wa kuanguka kwako, watakapougua waliojeruhiwa, yatakapofanyika machinjo kati yako.
Wote wakaao katika visiwa vile watakustaajabia, na wafalme wao wameogopa sana, wamefadhaika nyuso zao.
Bwana MUNGU asema hivi, Katika siku ile alipoteremka mpaka kuzimu niliamuru matanga, nilikifunika kilindi kwa ajili yake, nikiizuia mito yake, nayo maji makuu yalizuiwa; niliamuru Lebanoni kumwombolezea, na miti yote ya shambani ilizimia kwa ajili yake.