Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Ezekieli 23:46 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Maana Bwana MUNGU asema hivi; Nitaleta kusanyiko la watu juu yao, nami nitawatoa warushwe huku na huko, na kutekwa nyara.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Genge la watu litaletwa, litawatisha na kuwapora mali zao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Genge la watu litaletwa, litawatisha na kuwapora mali zao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Basi, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Genge la watu litaletwa, litawatisha na kuwapora mali zao.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Leteni watu wengi wenye makelele dhidi yao na uwaache wapate hofu na watekwe nyara.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo, Leteni watu wengi wenye makelele dhidi yao na uwaache wapate hofu na watekwe nyara.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Maana Bwana MUNGU asema hivi; Nitaleta kusanyiko la watu juu yao, nami nitawatoa warushwe huku na huko, na kutekwa nyara.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Ezekieli 23:46
9 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitawafanya kuwa kitu cha kutisha katika falme zote za duniani, kwa sababu ya Manase, mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa sababu ya mambo aliyoyatenda katika Yerusalemu.


Ee mlima wangu wa uwandani, nitatoa mali zako na hazina zako zote ziwe nyara, na mahali pako palipoinuka, kwa sababu ya dhambi, katika mipaka yako yote.


Naam, nitawatoa watupwe huku na huko katika falme zote za dunia, wapate mabaya; wawe kitu cha kulaumiwa, na mithali, na dhihaka, na laana, katika mahali pote nitakapowafukuzia.


angalieni, nitatuma watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyoko pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.


Nami nitawafuatia kwa upanga, na njaa, na tauni, nami nitawatoa watupwe huku na huko katika falme zote za dunia, wawe kitu cha kulaaniwa, na cha kushangaza, na cha kuzomewa, na cha kulaumiwa, katika mataifa yote nilikowafukuza.


Basi BWANA asema hivi, Hamkunisikiliza kumtangazia uhuru kila mtu ndugu yake, na kila mtu jirani yake; tazama, mimi nawatangazieni uhuru, asema BWANA, yaani, wa upanga, na njaa, na tauni; nami nitawatoa ninyi mtupwe huku na huko katika falme zote za dunia.


Tena wataleta mkutano wa watu juu yako, nao watakupiga kwa mawe, na kukuchoma kwa panga zao.


BWANA atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huku na huko katika falme zote za duniani.