Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Ezekieli 2:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la kitabu lilikuwa ndani yake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Nilipotazama, niliona nimenyoshewa mkono, na kumbe ulikuwa na kitabu kilichoandikwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Nilipotazama, niliona nimenyoshewa mkono, na kumbe ulikuwa na kitabu kilichoandikwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Nilipotazama, niliona nimenyoshewa mkono, na kumbe ulikuwa na kitabu kilichoandikwa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ndipo nikatazama, nami nikaona mkono ulionyooshwa kunielekea. Nao ulikuwa na kitabu,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ndipo nikatazama, nami nikaona mkono ulionyooshwa kunielekea. Nao ulikuwa na ukurasa wa kitabu,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la chuo lilikuwa ndani yake.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Ezekieli 2:9
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;


Twaa gombo la kitabu, ukaandike ndani yake maneno yote niliyokuambia juu ya Israeli, na juu ya Yuda, na juu ya mataifa yote, tangu siku ile niliponena nawe, tangu siku za Yosia, hata siku hii ya leo.


Kisha Yeremia akamwita Baruku, mwana wa Neria; naye Baruku akaandika katika gombo la kitabu maneno yote ya BWANA, yaliyotoka kinywani mwa Yeremia, ambayo BWANA alikuwa amemwambia.


Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha nenda ukaseme na wana wa Israeli.


Naye akanyosha mfano wa mkono, akanishika kwa kishungi kimoja cha nywele za kichwa changu; nayo roho ikaniinua kati ya dunia na mbingu, ikanileta katika maono ya Mungu mpaka Yerusalemu, mpaka mlango wa kuingilia ua wa ndani uelekeao upande wa kaskazini; mahali palipokuwa pamewekwa sanamu ya wivu, itiayo wivu.


Na tazama, mkono ukanigusa, ukaniweka juu ya magoti yangu, na viganja vya mikono yangu.


Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu, vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme, mahali palipokielekea kinara; naye mfalme akakiona kiganja cha ule mkono ulioandika.


Basi, nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la kitabu lirukalo.


Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atakatiwa mbali kama ilivyoandikwa upande, na kwa hiyo kila aapaye kwa uongo atakatiliwa mbali kama ilivyo andikwa upande wa pili.


Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la kitabu nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu.