Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, Nao watoto wa simba jike wametawanyika mbalimbali.
Ezekieli 19:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC useme, Mama yako alikuwa nini? Simba mke; alijilaza kati ya simba, kati ya wanasimba aliwalisha watoto wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mama yenu alikuwa simba wa fahari miongoni mwa simba wengine. Alikaa kati ya simba vijana, akawalisha watoto wake. Biblia Habari Njema - BHND Mama yenu alikuwa simba wa fahari miongoni mwa simba wengine. Alikaa kati ya simba vijana, akawalisha watoto wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mama yenu alikuwa simba wa fahari miongoni mwa simba wengine. Alikaa kati ya simba vijana, akawalisha watoto wake. Neno: Bibilia Takatifu na useme: “ ‘Tazama jinsi gani mama yako alivyokuwa simba jike miongoni mwa simba! Alilala katikati ya wana simba na kulisha watoto wake. Neno: Maandiko Matakatifu na useme: “ ‘Tazama jinsi gani mama yako alivyokuwa simba jike miongoni mwa simba! Alilala katikati ya wana simba na kulisha watoto wake. BIBLIA KISWAHILI useme, Mama yako alikuwa nini? Simba mke; alijilaza kati ya simba, kati ya wanasimba aliwalisha watoto wake. |
Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, Nao watoto wa simba jike wametawanyika mbalimbali.
Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wanasimba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.
Akamlea mtoto mmoja katika watoto wake, akawa mwanasimba, akajifunza kuwinda mawindo, akala watu.
Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwanasimba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.
Sikiza, maombolezo ya wachungaji, Kwa maana utukufu wao umeharibiwa; Sikiza, ngurumo za simba, Kwa maana vichaka vya Yordani vimeharibiwa!