Wakawapitisha watoto wao, wa kiume na wa kike, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza wenyewe wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.
Ezekieli 16:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC hata ukawaua watoto wangu, na kuwatoa kwa kuwapitisha motoni kwa hao? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, jambo hili la kuwachinja watoto wangu ili wawe tambiko ya kuteketeza kwa ajili ya sanamu zako ni jambo dogo? Biblia Habari Njema - BHND Je, jambo hili la kuwachinja watoto wangu ili wawe tambiko ya kuteketeza kwa ajili ya sanamu zako ni jambo dogo? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, jambo hili la kuwachinja watoto wangu ili wawe tambiko ya kuteketeza kwa ajili ya sanamu zako ni jambo dogo? Neno: Bibilia Takatifu Uliwachinja watoto wangu na kuwatoa kafara kwa sanamu. Neno: Maandiko Matakatifu Uliwachinja watoto wangu na kuwatoa kafara kwa sanamu. BIBLIA KISWAHILI hata ukawaua watoto wangu, na kuwatoa kwa kuwapitisha motoni kwa hao? |
Wakawapitisha watoto wao, wa kiume na wa kike, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza wenyewe wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.
Akampitisha mwanawe motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.
Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki.
Tena akafukiza uvumba katika bonde la mwana wa Hinomu, akawateketeza wanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.
Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli, wa binadamu na wa mnyama; ni wangu huyo.
nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu;
nami nikawatia unajisi kwa matoleo yao wenyewe, kwa kuwa walipitisha motoni wote waliofungua tumbo; ili kuwafanya kuwa ukiwa, wakapate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Usimtoe kafara mzawa wako yeyote kwa Moleki na ulinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.
Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,