Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubirie watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
Ezekieli 16:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Wewe mtu, ujulishe mji wa Yerusalemu machukizo yake. Biblia Habari Njema - BHND “Wewe mtu, ujulishe mji wa Yerusalemu machukizo yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Wewe mtu, ujulishe mji wa Yerusalemu machukizo yake. Neno: Bibilia Takatifu “Mwanadamu, kabili Yerusalemu kuhusu matendo yake ya kuchukiza, Neno: Maandiko Matakatifu “Mwanadamu, ijulishe Yerusalemu kuhusu mwenendo wake wa machukizo BIBLIA KISWAHILI Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake, |
Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubirie watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti.
Na wewe, mwanadamu, je! Utauhukumu, utauhukumu mji huu wa damu? Basi uujulishe machukizo yake yote.
Tena BWANA akaniambia, Mwanadamu, utawahukumu Ohola na Oholiba? Basi watangazie matendo yao maovu.
Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya BWANA; kwa sababu wamelivunja agano langu, wameiasi sheria yangu.