Ezekieli 15:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, watupwa motoni kuwa kuni moto unapoziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yoyote? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huo wafaa tu kuwashia moto. Tena moto unapoteketeza sehemu yake ya mwanzo na ya mwisho na kuikausha sehemu ya katikati, je, hiyo yafaa kwa kitu chochote? Biblia Habari Njema - BHND Huo wafaa tu kuwashia moto. Tena moto unapoteketeza sehemu yake ya mwanzo na ya mwisho na kuikausha sehemu ya katikati, je, hiyo yafaa kwa kitu chochote? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huo wafaa tu kuwashia moto. Tena moto unapoteketeza sehemu yake ya mwanzo na ya mwisho na kuikausha sehemu ya katikati, je, hiyo yafaa kwa kitu chochote? Neno: Bibilia Takatifu Nao baada ya kutiwa motoni kama nishati na moto ukateketeza ncha zote mbili na kuunguza sehemu ya kati, je, unafaa kwa lolote? Neno: Maandiko Matakatifu Nao baada ya kutiwa motoni kama nishati na moto ukateketeza ncha zote mbili na kuunguza sehemu ya kati, je, unafaa kwa lolote? BIBLIA KISWAHILI Tazama, watupwa motoni kuwa kuni moto unapoziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yoyote? |
Na mtu hodari atakuwa kama makumbi, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima.
Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yoyote? Watu waweza kufanya chango kwa huo, ili kutundika chombo chochote?
Tazama, ulipokuwa mzima, haukufaa kwa kazi yoyote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yoyote?
Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mzabibu kati ya miti ya msituni, niliyoupa moto uwe kuni, ndivyo nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu.
Na moto umetoka katika vijiti vya matawi yake, umekula matunda yake, hata hana tena kijiti cha nguvu kifaacho kwa fimbo ya enzi ya kutawala. Na hayo ni maombolezo, nayo yatakuwa maombolezo.
Baadhi yenu nimewaangamiza, kama hapo Mungu alipoiangamiza Sodoma na Gomora, nanyi mkawa kama kinga kilichonyakuliwa motoni; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.