Nikatambua, na tazama, si Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; kwa kuwa Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri.
Ezekieli 13:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Hamkuona maono ya bure, hamkunena ubashiri wa uongo? Nanyi mwasema, BWANA asema; ila mimi sikusema neno. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, nawaulizeni: Je, maono yenu si uongo mtupu na utabiri wenu udanganyifu? Nyinyi mnadai kwamba mnasema kwa jina langu hali mimi sijaongea nanyi kamwe! Biblia Habari Njema - BHND Basi, nawaulizeni: Je, maono yenu si uongo mtupu na utabiri wenu udanganyifu? Nyinyi mnadai kwamba mnasema kwa jina langu hali mimi sijaongea nanyi kamwe! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, nawaulizeni: Je, maono yenu si uongo mtupu na utabiri wenu udanganyifu? Nyinyi mnadai kwamba mnasema kwa jina langu hali mimi sijaongea nanyi kamwe! Neno: Bibilia Takatifu Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu, hapo msemapo, “Mwenyezi Mungu asema”, wakati Mimi sijasema? Neno: Maandiko Matakatifu Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu hapo msemapo, “bwana asema,” lakini Mimi sijasema? BIBLIA KISWAHILI Je! Hamkuona maono ya bure, hamkunena ubashiri wa uongo? Nanyi mwasema, BWANA asema; ila mimi sikusema neno. |
Nikatambua, na tazama, si Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; kwa kuwa Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri.
wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
Wameona ubatili, na uganga wa uongo, hao wasemao, BWANA asema; lakini BWANA hakuwatuma; nao wamewapa watu tumaini ya kuwa neno lile litatimizwa.
Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiwa na maono ya udanganyifu, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo BWANA hakusema neno.
Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo watu wanatangatanga kama kondoo, wanateseka kwa kukosa mchungaji.