Ezekieli 11:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ninyi mmeuogopa upanga; nami nitauleta upanga juu yenu, asema Bwana MUNGU. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyinyi mmeogopa upanga? Basi, mimi nitaleta upanga dhidi yenu! Biblia Habari Njema - BHND Nyinyi mmeogopa upanga? Basi, mimi nitaleta upanga dhidi yenu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyinyi mmeogopa upanga? Basi, mimi nitaleta upanga dhidi yenu! Neno: Bibilia Takatifu Mnaogopa upanga, nao upanga huo ndio nitakaouleta dhidi yenu, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Neno: Maandiko Matakatifu Mnaogopa upanga, nao upanga huo ndio nitakaouleta juu yenu, asema bwana Mwenyezi. BIBLIA KISWAHILI Ninyi mmeuogopa upanga; nami nitauleta upanga juu yenu, asema Bwana MUNGU. |
Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu nilipoita, hawakuitika; na niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua nisiyoyafurahia.
Haya ndiyo yatakayowapata watu wote waelekezao nyuso zao kwenda Misri, na kukaa huko; watakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; hakuna mtu awaye yote miongoni mwao atakayesalia, au kuokoka katika mabaya nitakayoyaleta juu yao.
Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu.