Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubirie watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
Ezekieli 11:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi toa unabii juu yao, Ee mwanadamu, toa unabii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo, toa unabii dhidi yao! Tabiri ewe mtu!” Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo, toa unabii dhidi yao! Tabiri ewe mtu!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo, toa unabii dhidi yao! Tabiri ewe mtu!” Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo tabiri dhidi yao; tabiri, ewe mwanadamu.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo toa unabii dhidi yao, tabiri, Ewe mwanadamu.” BIBLIA KISWAHILI Basi toa unabii juu yao, Ee mwanadamu, toa unabii. |
Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubirie watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
Mwanadamu, uelekeze uso wako Yerusalemu, ukadondoze neno lako upande wa mahali patakatifu, ukatabiri juu ya nchi ya Israeli;
Kwa sababu hiyo nimewakatakata kwa vinywa vya manabii; nimewaua kwa maneno ya kinywa changu; na hukumu yangu itatokea kama mwanga.
Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya BWANA; kwa sababu wamelivunja agano langu, wameiasi sheria yangu.