Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi.
Ezekieli 10:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu, hapo walipotoka nje, nayo magurudumu yakawa kando yao; wakasimama mahali pa kuingilia pa mlango wa upande wa mashariki wa nyumba ya BWANA; na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Viumbe wakakunjua mabawa yao, wakapaa juu, mimi nikiwa nawaona na yale magurudumu yalikuwa kando yao. Wakasimama mbele ya lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. Biblia Habari Njema - BHND Viumbe wakakunjua mabawa yao, wakapaa juu, mimi nikiwa nawaona na yale magurudumu yalikuwa kando yao. Wakasimama mbele ya lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Viumbe wakakunjua mabawa yao, wakapaa juu, mimi nikiwa nawaona na yale magurudumu yalikuwa kando yao. Wakasimama mbele ya lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. Neno: Bibilia Takatifu Nilipokuwa nikitazama, makerubi wakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda, yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi Mungu; nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao. Neno: Maandiko Matakatifu Nilipokuwa nikitazama, makerubi yakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda, yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya bwana, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao. BIBLIA KISWAHILI Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu, hapo walipotoka nje, nayo magurudumu yakawa kando yao; wakasimama mahali pa kuingilia pa mlango wa upande wa mashariki wa nyumba ya BWANA; na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. |
Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi.
Tena roho ikaniinua, ikanileta hadi katika lango la upande wa mashariki mwa nyumba ya BWANA, lililoelekea upande wa mashariki; na tazama, mahali pa kuingilia pa lango walikuwako watu ishirini na watano; na katikati yao nikamwona Yaazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, nao ni wakuu wa watu.
na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling'aa kwa utukufu wake.
Na huo utukufu wa BWANA ukaingia ndani ya nyumba, kwa njia ya lango lile lielekealo upande wa mashariki.
Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya BWANA, na tazama, mlangoni pa hekalu la BWANA, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la BWANA, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki.