Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Ezekieli 10:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha huo utukufu wa BWANA ukatoka pale juu ya kizingiti cha nyumba, ukasimama juu ya makerubi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulitoka kwenye kizingiti cha nyumba, ukaenda na kusimama juu ya wale viumbe. Biblia Habari Njema - BHND Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulitoka kwenye kizingiti cha nyumba, ukaenda na kusimama juu ya wale viumbe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulitoka kwenye kizingiti cha nyumba, ukaenda na kusimama juu ya wale viumbe. Neno: Bibilia Takatifu Kisha utukufu wa Mwenyezi Mungu ukaondoka pale kwenye kizingiti cha Hekalu na kusimama juu ya wale makerubi. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha utukufu wa bwana ukaondoka pale kwenye kizingiti cha Hekalu na kusimama juu ya wale makerubi. BIBLIA KISWAHILI Kisha huo utukufu wa BWANA ukatoka pale juu ya kizingiti cha nyumba, ukasimama juu ya makerubi. |
Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.
Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Akiwa katika giza la mawingu mazito yaliyojaa maji.
Uonyeke, Ee Yerusalemu, nafsi yangu, isije ikafarakana nawe; nisije nikakufanya ukiwa, nchi isiyokaliwa na watu.
Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nilikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huku na huko kati ya mawe ya moto.
na vizingiti, na madirisha yaliyofungwa, na baraza za pande zote za ghorofa zile tatu, zilizokikabili kizingiti, zilitiwa mabamba ya mti pande zote; na toka chini hadi madirishani; (nayo madirisha yamefunikwa);
na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling'aa kwa utukufu wake.
Akaniambia, Mwanadamu, je! Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, ili niende zangu mbali na patakatifu pangu? Lakini utaona tena machukizo makubwa mengine.
Wajapolea watoto wao, mimi nitawanyang'anya watoto wao, asisalie hata mtu mmoja; naam, ole wao! Nitakapoondoka na kuwaacha.
Bwana wake akaondoka asubuhi, akaifungua milango ya nyumba, akatoka nje ili aende zake, na tazama, huyo mwanamke suria wake alikuwa ameanguka pale mlangoni pa nyumba, na mikono yake ilikuwa iko pale kizingitini.