Basi, nilipokuwa nikivitazama wale viumbe hai, tazama, gurudumu moja juu ya nchi, karibu na kila kimoja cha wale viumbe hai, pande zake zote nne.
Ezekieli 10:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na magurudumu hayo yaliitwa Kisulisuli, nami nilisikia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Niliambiwa kuwa magurudumu yale yanaitwa, “Magurudumu Yanayozunguka.” Biblia Habari Njema - BHND Niliambiwa kuwa magurudumu yale yanaitwa, “Magurudumu Yanayozunguka.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Niliambiwa kuwa magurudumu yale yanaitwa, “Magurudumu Yanayozunguka.” Neno: Bibilia Takatifu Nikasikia magurudumu yakiitwa “magurudumu ya kisulisuli”. Neno: Maandiko Matakatifu Nikasikia magurudumu yakiitwa, “Magurudumu ya kisulisuli.” BIBLIA KISWAHILI Na magurudumu hayo yaliitwa Kisulisuli, nami nilisikia. |
Basi, nilipokuwa nikivitazama wale viumbe hai, tazama, gurudumu moja juu ya nchi, karibu na kila kimoja cha wale viumbe hai, pande zake zote nne.
Na mwili wao mzima, na maungo yao, na mikono yao, na mabawa yao, na magurudumu, wamejaa macho pande zote, hata magurudumu waliyokuwa nayo wale wanne.
Kila mmoja alikuwa na nyuso nne; uso wa kwanza ulikuwa uso wa kerubi, na uso wa pili ulikuwa uso wa mwanadamu, na uso wa tatu ulikuwa uso wa simba, na uso wa nne ulikuwa uso wa tai.
Naye akamwambia mtu yule aliyevaa bafta, akasema, Ingia kati ya magurudumu yazungukayo, yaani, chini ya kerubi, ukaijaze mikono yako yote miwili makaa ya moto, toka katikati ya makerubi, ukayamwage juu ya mji. Akaingia ndani mbele ya macho yangu.