Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Ezekieli 1:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Na viumbe hao walipokwenda, magurudumu yalikwenda kandokando yao, na viumbe hao walipoinuliwa, magurudumu nayo yaliinuliwa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Hao viumbe hai walipokwenda, magurudumu nayo yalikwenda kandokando yao; na viumbe hao walipoinuka juu kutoka ardhini, magurudumu hayo yaliinuka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Hao viumbe hai walipokwenda, magurudumu nayo yalikwenda kandokando yao; na viumbe hao walipoinuka juu kutoka ardhini, magurudumu hayo yaliinuka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Hao viumbe hai walipokwenda, magurudumu nayo yalikwenda kandokando yao; na viumbe hao walipoinuka juu kutoka ardhini, magurudumu hayo yaliinuka.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wale viumbe hai walipoenda, magurudumu yaliyokuwa kando yao yalisogea; wakati hao viumbe hai walipoinuka kutoka ardhini, magurudumu nayo yaliinuka.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Vile viumbe hai vilipokwenda, magurudumu yaliyokuwa kando yao yalisogea na wakati hivyo viumbe hai vilipoinuka kutoka ardhini magurudumu nayo yaliinuka.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na viumbe hao walipokwenda, magurudumu yalikwenda kandokando yao, na viumbe hao walipoinuliwa, magurudumu nayo yaliinuliwa.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Ezekieli 1:19
5 Marejeleo ya Msalaba  

Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.

Basi, nilipokuwa nikivitazama wale viumbe hai, tazama, gurudumu moja juu ya nchi, karibu na kila kimoja cha wale viumbe hai, pande zake zote nne.

Walipokwenda hao, yalikwenda hayo nayo; na waliposimama hao, yalisimama hayo nayo; na walipoinuliwa hao juu ya nchi, magurudumu yaliinuliwa karibu nao; maana roho ya viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu.

Na makerubi walipokwenda, magurudumu yale yalikwenda kando yao; na makerubi walipoinua mabawa yao, wapate kupaa juu kutoka katika dunia, magurudumu yale hayakugeuka wala kutoka kando yao.

Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu, hapo walipotoka nje, nayo magurudumu yakawa kando yao; wakasimama mahali pa kuingilia pa mlango wa upande wa mashariki wa nyumba ya BWANA; na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.