Basi kulikuwa na vita siku nyingi kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi; Daudi akaendelea akasitawi, lakini nyumba ya Sauli ikaendelea kudhoofika.
Esta 9:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana Mordekai alikuwa mkuu nyumbani mwa mfalme, na sifa yake imevuma katika mikoa yote, kwa kuwa huyo Mordekai amezidi kukuzwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mordekai sasa alikuwa mtu mwenye madaraka makubwa katika ikulu, na habari zake zilienea katika mikoa yote kwamba uwezo wake ulikuwa unazidi kuongezeka. Biblia Habari Njema - BHND Mordekai sasa alikuwa mtu mwenye madaraka makubwa katika ikulu, na habari zake zilienea katika mikoa yote kwamba uwezo wake ulikuwa unazidi kuongezeka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mordekai sasa alikuwa mtu mwenye madaraka makubwa katika ikulu, na habari zake zilienea katika mikoa yote kwamba uwezo wake ulikuwa unazidi kuongezeka. Neno: Bibilia Takatifu Mordekai alikuwa mtu mashuhuri katika jumba la mfalme; sifa zake zilienea katika majimbo yote naye alipata uwezo zaidi na zaidi. Neno: Maandiko Matakatifu Mordekai alikuwa mtu mashuhuri katika jumba la mfalme; sifa zake zilienea katika majimbo yote naye alipata uwezo zaidi na zaidi. Swahili Roehl Bible 1937 Kwani Mordekai alikuwa mkubwa katika nyumba ya mfalme, nayo sifa yake ikasikilika katika majimbo yote, kwani huyo mtu Mordekai akaendelea kuwa mkubwa zaidi. |
Basi kulikuwa na vita siku nyingi kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi; Daudi akaendelea akasitawi, lakini nyumba ya Sauli ikaendelea kudhoofika.
Naye Daudi akaendelea, akazidi kuwa mkuu; kwa maana BWANA wa majeshi alikuwa pamoja naye.
Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Umedi na Uajemi?
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Umeniokoa kutoka kwa mashindano ya watu, Umenifanya niwe kichwa cha mataifa. Watu nisiowajua walinitumikia.
BWANA akawapa watu hao kibali machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake.
Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya msifiwe na kujulikana, hao ambao aibu yao ilikuwa katika dunia yote.
Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nilisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau nitawadharau.