Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Esta 8:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme akaivua pete yake ya mhuri aliyokuwa amemnyanganya Hamani, akampa Mordekai. Esta naye akampa Mordekai mamlaka juu ya mali ya Hamani. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme akaivua pete yake ya mhuri aliyokuwa amemnyanganya Hamani, akampa Mordekai. Esta naye akampa Mordekai mamlaka juu ya mali ya Hamani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme akaivua pete yake ya mhuri aliyokuwa amemnyang'anya Hamani, akampa Mordekai. Esta naye akampa Mordekai mamlaka juu ya mali ya Hamani. Neno: Bibilia Takatifu Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyang’anya Hamani, akampa Mordekai, naye Esta akamweka Mordekai asimamie shamba la Hamani. Neno: Maandiko Matakatifu Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyang’anya Hamani, akampa Mordekai, naye Esta akamweka Mordekai juu ya shamba la Hamani. Swahili Roehl Bible 1937 Ndipo, mfalme alipoondoa kidoleni pete yake yenye muhuri, aliyomvua Hamani, akampa Mordekai. Naye Esteri akamkalisha Mordekai katika nyumba ya Hamani. |
Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Umedi na Uajemi?
Ndipo mfalme alipoivua pete yake ya kupigia mhuri kutoka mkononi, akampa Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.
Tena Esta akasema na mfalme mara ya pili, akaanguka miguuni pake, akamsihi kwa machozi ayaondoe madhara ya Hamani, Mwagagi, na shauri alilowafanyia Wayahudi.
Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya utawala wote wa Babeli, na kuwa mtawala mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.
Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;