Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Esta 8:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Ikawa nuru na furaha na shangwe na heshima kwa Wayahudi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Hapo Wayahudi waliona fahari, heshima na furaha, wakajisikia wenye nafuu na ushindi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Hapo Wayahudi waliona fahari, heshima na furaha, wakajisikia wenye nafuu na ushindi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Hapo Wayahudi waliona fahari, heshima na furaha, wakajisikia wenye nafuu na ushindi.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa maana kwa Wayahudi ulikuwa wakati wa raha na furaha, shangwe na heshima.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa maana kwa Wayahudi ulikuwa wakati wa raha na furaha, shangwe na heshima.

Tazama sura

Swahili Roehl Bible 1937

Hivyo ndivyo, Wayuda walivyopata machangamko na furaha na macheko na macheo.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Esta 8:16
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nenda ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Susa, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.


Hii ndiyo siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari; na siku ya kumi na nne ya mwezi huo wakapumzika, wakaifanya kuwa siku ya karamu na furaha.


Nuru huwaangaza wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki.


BWANA ndiye aliye Mungu, Naye ndiye aliyetupa nuru. Ifungeni dhabihu kwa kamba Pembeni mwa madhabahu.


Kwa kuwa Wewe unaiwasha taa yangu; BWANA Mungu wangu aniangazia giza langu.


Ili nafsi yangu ikusifu, Wala isinyamaze. Ee BWANA, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.


Nuru humwangazia mwenye haki, Na furaha ni kwa wanyofu wa moyo.


Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu wanapoangamia, watu hushangilia.


Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha.


Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitatoweka.