Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.
Esta 7:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi mfalme na Hamani walikwenda kula karamu pamoja na malkia Esta. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo mfalme na Hamani wakaenda kula karamu na malkia Esta. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo mfalme na Hamani wakaenda kula karamu na malkia Esta. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo mfalme na Hamani wakaenda kula karamu na malkia Esta. Neno: Bibilia Takatifu Basi mfalme na Hamani wakaenda kula chakula pamoja na Malkia Esta. Neno: Maandiko Matakatifu Basi mfalme na Hamani wakaenda kula chakula pamoja na Malkia Esta. Swahili Roehl Bible 1937 Mfalme akaja pamoja na Hamani karamuni kwake Esteri, mkewe mfalme. |
Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.
Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunitimizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema.
Walipokuwa wangali wakisema naye, matowashi wa mfalme walifika, wakahimiza kumleta Hamani katika karamu ile aliyoiandaa Esta.
Mfalme akamwambia Esta tena siku ya pili pale pale penye karamu ya divai, Malkia Esta, dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utatimiziwa.