Tena, wakati wa kutawala kwake Ahasuero, mwanzo wa kutawala kwake, watu wakaandika mashitaka juu ya wenyeji wa Yuda na Yerusalemu.
Esta 6:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikaonekana kuwa imeandikwa ya kwamba Mordekai aliwasema Bigthana na Tereshi, wasimamizi wawili wa mfalme, katika hao waliolinda mlango, waliotaka kumwua mfalme Ahasuero. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikaonekana ilivyoandikwa jinsi Mordekai alivyongamua njama ya kumwua mfalme iliyokuwa imefanywa na Bigthana na Tereshi, wawili kati ya matowashi wa mfalme waliokuwa walinzi wa vyumba vya mfalme. Biblia Habari Njema - BHND Ikaonekana ilivyoandikwa jinsi Mordekai alivyongamua njama ya kumwua mfalme iliyokuwa imefanywa na Bigthana na Tereshi, wawili kati ya matowashi wa mfalme waliokuwa walinzi wa vyumba vya mfalme. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikaonekana ilivyoandikwa jinsi Mordekai alivyong'amua njama ya kumwua mfalme iliyokuwa imefanywa na Bigthana na Tereshi, wawili kati ya matowashi wa mfalme waliokuwa walinzi wa vyumba vya mfalme. Neno: Bibilia Takatifu Ikaonekana imeandikwa humo kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumuua Mfalme Ahasuero. Neno: Maandiko Matakatifu Kitabu hicho kilikutwa na kumbukumbu kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumuua Mfalme Ahasuero. Swahili Roehl Bible 1937 zikaoneka zile habari zilizoandikwa za kwamba: Mordekai ameumbua watumishi wa nyumbani mwa mfalme, Bigitana na Teresi, waliokuwa walinda mlango, waliotafuta njia ya kumwua mfalme Ahaswerosi kwa mikono yao. |
Tena, wakati wa kutawala kwake Ahasuero, mwanzo wa kutawala kwake, watu wakaandika mashitaka juu ya wenyeji wa Yuda na Yerusalemu.
Mfalme akasema, Je! Ni heshima gani au hadhi gani Mordekai aliyofanyiwa kwa ajili ya hayo? Watumishi wa mfalme waliomhudumia wakamwambia, Hakuna alilofanyiwa.