Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo, akanywa.
Esta 5:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Esta akasema, Mfalme akiona vema, na aje leo, mfalme na Hamani, kwenye karamu niliyomwandalia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Esta akamjibu, “Ukipenda, ewe mfalme, uje leo pamoja na Hamani, kwenye karamu ninayoandaa kwa ajili yako, mfalme.” Biblia Habari Njema - BHND Esta akamjibu, “Ukipenda, ewe mfalme, uje leo pamoja na Hamani, kwenye karamu ninayoandaa kwa ajili yako, mfalme.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Esta akamjibu, “Ukipenda, ewe mfalme, uje leo pamoja na Hamani, kwenye karamu ninayoandaa kwa ajili yako, mfalme.” Neno: Bibilia Takatifu Esta akajibu, “Kama itampendeza mfalme, mfalme pamoja na Hamani waje leo katika karamu niliyomwandalia.” Neno: Maandiko Matakatifu Esta akajibu, “Kama itampendeza mfalme, mfalme pamoja na Hamani waje leo katika karamu ambayo nimeiandaa kwa ajili yake.” Swahili Roehl Bible 1937 Esteri akamjibu: Kama ni vizuri kwake mfalme, mfalme na aje leo pamoja na Hamani kula karamu, Esteri aliyomfanyizia. |
Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo, akanywa.
Tena semeni, Tazama, mtumwa wako, Yakobo, yuko nyuma yetu. Maana alisema, Nitamsuluhisha kwa zawadi inayonitangulia, baadaye nitamwona uso wake; huenda atanikubali uso wangu.
Naye Vashti, malkia, akawafanyia karamu wanawake ndani ya nyumba ya kifalme ya mfalme Ahasuero.
Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.
Mfalme akamwambia, malkia Esta, unataka nini? Nayo ni haja gani uliyo nayo? Utapewa hata nusu ya ufalme.
Basi mfalme akasema, Mhimize Hamani, ili ifanyike kama Esta alivyoomba. Hivyo mfalme na Hamani wakafika katika karamu ile aliyoiandaa Esta.
Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunitimizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema.
Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu muwe watu wazima.