Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Esta 3:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta elfu kumi za fedha mikononi mwa watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Ukipenda, ewe mfalme, amri na itolewe, watu hawa waangamizwe. Nami naahidi, kama utaamuru hivyo, nitatoa kiasi cha kilo 10,000 za fedha ziwekwe katika hazina ya mfalme.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Ukipenda, ewe mfalme, amri na itolewe, watu hawa waangamizwe. Nami naahidi, kama utaamuru hivyo, nitatoa kiasi cha kilo 10,000 za fedha ziwekwe katika hazina ya mfalme.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Ukipenda, ewe mfalme, amri na itolewe, watu hawa waangamizwe. Nami naahidi, kama utaamuru hivyo, nitatoa kiasi cha kilo 10,000 za fedha ziwekwe katika hazina ya mfalme.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kama inampendeza mfalme, itolewe amri kuwaangamiza, nami nitaweka talanta elfu kumi za fedha katika hazina ya mfalme kwa ajili ya watu watakaoshughulikia jambo hili.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kama inampendeza mfalme, itolewe amri kuwaangamiza, nami nitaweka talanta 10,000 za fedha katika hazina ya mfalme kwa ajili ya watu watakaoshughulikia jambo hili.”

Tazama sura

Swahili Roehl Bible 1937

Ikiwa, mfalme avione kuwa vema, na viandikwe kwamba: Watu na wawaangamize! Kisha mimi nitawapimia wenye kazi hiyo mikononi mwao mizigo ya fedha elfu kumi, waipeleke na kuitia katika malimbiko ya mfalme.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Esta 3:9
7 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akakubali maneno ya Efroni. Abrahamu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara.


Ndipo mfalme alipoivua pete yake ya kupigia mhuri kutoka mkononi, akampa Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.


Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna watu wa taifa moja waliotawanyika na kukaa kila mahali katikati ya watu wa mataifa walioko katika mikoa yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimetofautiana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.


Naye Mordekai akamweleza yote yaliyompata, na hesabu ya fedha Hamani aliahidi kulipa katika hazina ya mfalme, ili Wayahudi waangamizwe.


Maana tumeuzwa, mimi na watu wangu, ili tuharibiwe, na kuuawa, na kuangamia. Kama tungaliuzwa kuwa watumwa na wajakazi, ningalinyamaza; japo hata hivyo adui asingeweza kufidia hasara ya mfalme.


Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia, wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi.


Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja mwenye deni la talanta elfu kumi.