Bali Vashti, malkia, hakutii amri ya mfalme, alikataa kuja kama alivyoamriwa na mfalme kupitia kwa matowashi; kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, na hasira yake ikawaka ndani yake.
Esta 3:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hamwinamii wala kumsujudia, alighadhibika sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hamani aliwaka hasira alipojua kwamba Mordekai hamwinamii wala hamsujudii. Biblia Habari Njema - BHND Hamani aliwaka hasira alipojua kwamba Mordekai hamwinamii wala hamsujudii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hamani aliwaka hasira alipojua kwamba Mordekai hamwinamii wala hamsujudii. Neno: Bibilia Takatifu Hamani alipoona kuwa Mordekai hampigii magoti wala kumpa heshima, alighadhibika. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati Hamani alipoona kuwa Mordekai hampigii magoti wala kumpa heshima alighadhibika. Swahili Roehl Bible 1937 Hamani alipoona, ya kuwa Mordekai hampigii magoti, wala hamwangukii, ndipo, makali yenye moto yalipomjaa Hamani moyoni. |
Bali Vashti, malkia, hakutii amri ya mfalme, alikataa kuja kama alivyoamriwa na mfalme kupitia kwa matowashi; kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, na hasira yake ikawaka ndani yake.
Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi langoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo mfalme alivyoamuru wamfanyie. Lakini Mordekai hakumwinamia, wala kumsujudia.
Ikawa, waliposema naye kila siku asiwasikilize, wakamwarifu Hamani, ili kuona kama mambo yake Mordekai yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa yeye ni Myahudi.
Basi Hamani alitoka siku ile kwa furaha na ukunjufu wa moyo; lakini Hamani alipomwona Mordekai mlangoni pa mfalme, ya kwamba hasimami wala kunyenyekea mbele yake, alijaa ghadhabu juu ya Mordekai.
Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
Ndipo Nebukadneza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuri mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto.