Na yule Mordekai akawa akitembea kila siku mbele ya ua wa nyumba ya wanawake, ili ajue hali yake Esta, na yale yatakayompata.
Esta 2:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC mwanamwali huingia hivyo kwa mfalme; kila alichotaka alipewa kwenda nacho kutoka katika nyumba ya wanawake ili kuingia katika nyumba ya mfalme. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati wa kwenda kwa mfalme, kila mwali alipewa kila alichotaka kuchukua kutoka nyumba ya wanawake kwenda nacho ikulu. Biblia Habari Njema - BHND Wakati wa kwenda kwa mfalme, kila mwali alipewa kila alichotaka kuchukua kutoka nyumba ya wanawake kwenda nacho ikulu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati wa kwenda kwa mfalme, kila mwali alipewa kila alichotaka kuchukua kutoka nyumba ya wanawake kwenda nacho ikulu. Neno: Bibilia Takatifu Basi hivi ndivyo ambavyo msichana angeingia kwa mfalme: Kila kitu alichohitaji aliruhusiwa kuchukua kutoka nyumba ya wanawake na kwenda navyo katika jumba la mfalme. Neno: Maandiko Matakatifu Basi hivi ndivyo ambavyo msichana angeingia kwa mfalme: Kila kitu alichohitaji aliruhusiwa kuchukua kutoka nyumba ya wanawake na kwenda navyo katika jumba la mfalme. Swahili Roehl Bible 1937 Basi, hayo yalipokwisha, kila mara kijana alipoingia kwa mfalme hupewa yote, aliyoyataka kwenda nayo kutoka mle nyumbani mwa wanawake kuingia nyumbani mwa mfalme. |
Na yule Mordekai akawa akitembea kila siku mbele ya ua wa nyumba ya wanawake, ili ajue hali yake Esta, na yale yatakayompata.
Basi zamu ya kila mwanamwali kuingia kwa mfalme Ahasuero, iliwadia baada ya kutayarishwa kulingana na sheria ya wanawake kwa miezi kumi na miwili; kwa kuwa ndivyo zilivyotimia siku zao za utakaso, miezi sita kwa mafuta ya manemane, na miezi sita kwa manukato na vifaa vya utakaso wa wanawake;
Huenda jioni, na asubuhi hurudi katika nyumba ya pili ya wanawake, mikononi mwa Shaashgazi, msimamizi wake mfalme, aliyewalinda masuria. Wala haingii tena kwa mfalme, isipokuwa awe amempendeza mfalme, naye akaitwa kwa jina.