Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
Esta 10:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme Ahasuero alitoza kodi watu wa bara na pwani. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme Ahasuero alitoza kodi watu wa bara na pwani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme Ahasuero alitoza kodi watu wa bara na pwani. Neno: Bibilia Takatifu Mfalme Ahasuero alitoza ushuru katika himaya yake yote, hadi miambao yake ya mbali. Neno: Maandiko Matakatifu Mfalme Ahasuero alitoza ushuru katika ufalme wake wote hadi kwenye miambao yake ya mbali. Swahili Roehl Bible 1937 Mfalme Ahaswerosi akatoza kodi katika hiyo nchi, hata katika visiwa vya baharini. |
Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
Katika nyakati za Ahasuero; Ahasuero aliyetawala mikoa mia moja ishirini na saba, kutoka India mpaka Kushi;
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na wakuu wa tarafa na wakuu wa mikoa kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi, mikoa mia moja na ishirini na saba, kila mkoa kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao.
Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.
Basi, mtukuzeni BWANA katika mashariki, litukuzeni jina la BWANA, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari.
Baada ya hayo atauelekeza uso wake kwenye visiwa, naye atavipiga visiwa vingi; lakini mkuu mmoja ataikomesha aibu iliyoletwa na yeye; naam, aibu yake hiyo atamrudishia mwenyewe.
Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.