Danieli 5:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. Biblia Habari Njema - BHND TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. Neno: Bibilia Takatifu “Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na kuonekana umepungua. Neno: Maandiko Matakatifu “Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua. Swahili Roehl Bible 1937 Tekel ni kwamba: Umepimwa kwa mizani, ukaoneka kuwa mwepesi. |
Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo.
Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.
Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.