Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
Amosi 9:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao wajapojificha katika kilele cha Karmeli, nitawatafuta na kuwatoa toka huko; na wajapositirika katika vilindi vya bahari nisiwaone, nitamwagiza joka huko, naye atawauma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wajapojificha juu ya mlima Karmeli, huko nitawasaka na kuwachukua; wajapojificha mbali nami vilindini mwa bahari, humo nitaliamuru joka la baharini liwaume. Biblia Habari Njema - BHND Wajapojificha juu ya mlima Karmeli, huko nitawasaka na kuwachukua; wajapojificha mbali nami vilindini mwa bahari, humo nitaliamuru joka la baharini liwaume. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wajapojificha juu ya mlima Karmeli, huko nitawasaka na kuwachukua; wajapojificha mbali nami vilindini mwa bahari, humo nitaliamuru joka la baharini liwaume. Neno: Bibilia Takatifu Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli, huko nitawawinda na kuwakamata. Wajapojificha uso wangu katika vilindi vya bahari, huko nako nitaamuru joka kuwauma. Neno: Maandiko Matakatifu Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli, huko nitawawinda na kuwakamata. Wajapojificha kutoka kwenye uso wangu katika vilindi vya bahari, huko nako nitaamuru joka kuwauma. BIBLIA KISWAHILI Nao wajapojificha katika kilele cha Karmeli, nitawatafuta na kuwatoa toka huko; na wajapositirika katika vilindi vya bahari nisiwaone, nitamwagiza joka huko, naye atawauma. |
Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu Lewiathani, nyoka yule mwepesi, na Lewiathani, nyoka yule mwenye kuzongazonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
Tazama, asema BWANA, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.
Naye alisema, BWANA atanguruma toka Sayuni, Atatoa sauti yake toka Yerusalemu; Na malisho ya wachungaji yatakauka, Na kilele cha Karmeli kitanyauka.