Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
2 Wathesalonike 3:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini msimtendee mtu huyo kama adui, bali mwonyeni kama ndugu. Biblia Habari Njema - BHND Lakini msimtendee mtu huyo kama adui, bali mwonyeni kama ndugu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini msimtendee mtu huyo kama adui, bali mwonyeni kama ndugu. Neno: Bibilia Takatifu Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. BIBLIA KISWAHILI lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. |
Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
Na ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.
Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu, (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha), sitatahayarika;
Kwa sababu hiyo, naandika haya nikiwa mbali nanyi, ili, nikija, nisiwe na ukali wa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.
Ndugu zangu, mtu akishikwa katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
Ndugu, tunawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote.
Ndugu, tunawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu kutoka kwa kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.