2 Wathesalonike 3:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini nyinyi ndugu, msichoke kutenda mema. Biblia Habari Njema - BHND Lakini nyinyi ndugu, msichoke kutenda mema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini nyinyi ndugu, msichoke kutenda mema. Neno: Bibilia Takatifu Lakini kwenu ninyi, ndugu, kamwe msichoke katika kutenda mema. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa upande wenu, ndugu, ninyi kamwe msichoke katika kutenda mema. BIBLIA KISWAHILI Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema. |
Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA.
wale ambao kwa subira katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoharibika, watapewa uzima wa milele;
Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
Tena maofisa na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake.
Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;
Iliyobaki, ndugu, tunawasihi na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.
Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili upinzani mkuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.
tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau maonyo ya Bwana, Wala usife moyo ukiadhibiwa naye;