Nanyi semeni, Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako.
2 Wakorintho 9:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani! Biblia Habari Njema - BHND Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani! Neno: Bibilia Takatifu Mungu apewe shukrani kwa karama yake isiyoelezeka! Neno: Maandiko Matakatifu Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka. BIBLIA KISWAHILI Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo. |
Nanyi semeni, Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako.
Mwimbieni BWANA zaburi, Enyi watauwa wake. Na kutoa shukrani. Kwa kukumbuka utakatifu wake.
naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuyainua makabila ya Yakobo, na kuwarejesha watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Yeye ambaye hakumhurumia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje pia kutupa chochote kingine pamoja naye?
Ila Mungu ashukuriwe, anayetufanya tushangilie ushindi daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.
Nao wenyewe, wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu.
na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,