Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.
2 Wakorintho 7:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Mungu, mwenye kuwapa shime wanyonge, alitupa moyo sisi pia kwa kuja kwake Tito. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Mungu, mwenye kuwapa shime wanyonge, alitupa moyo sisi pia kwa kuja kwake Tito. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Mungu, mwenye kuwapa shime wanyonge, alitupa moyo sisi pia kwa kuja kwake Tito. Neno: Bibilia Takatifu Bali Mungu, yeye awafarijie wenye huzuni, alitufariji kwa Tito kufika kwetu. Neno: Maandiko Matakatifu Bali Mungu, yeye awafarijie wenye huzuni, alitufariji kwa kufika kwake Tito. BIBLIA KISWAHILI Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito. |
Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.
Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani?
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia.
Ndipo bikira atafurahi katika kucheza, na vijana na wazee pamoja; maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha, nami nitawafariji, na kuwafurahisha waache huzuni zao.
Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunuia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa kufuata mfano wa Kristo Yesu;
Kwa hiyo tulifarijiwa. Tena katika kufarijiwa kwetu tulifurahi sana kupita kiasi kwa sababu ya furaha ya Tito; maana roho yake imeburudishwa na ninyi nyote.
Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lolote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.
Wala si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu habari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hata nikazidi kufurahi.
Basi ikiwako faraja yoyote katika Kristo, yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi, ukiwako ushirika wowote wa Roho, ikiwako huruma yoyote na rehema,
Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji katika imani yenu;