2 Wakorintho 3:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi “Bwana” ndiye Roho; lakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapa “Bwana” ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipo ulipo uhuru. Biblia Habari Njema - BHND Hapa “Bwana” ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipo ulipo uhuru. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapa “Bwana” ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipo ulipo uhuru. Neno: Bibilia Takatifu Basi Bwana Isa ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi, hapo pana uhuru. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Bwana Isa ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Mwenyezi Mungu, hapo pana uhuru. BIBLIA KISWAHILI Basi “Bwana” ndiye Roho; lakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. |
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa kiumbe aliye hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.