Lakini desturi ya Musa ilikuwa alipoingia mbele za BWANA kusema naye, kuuvua huo utaji mpaka atoke; akatoka akawaambia wana wa Israeli maneno yote aliyoambiwa.
2 Wakorintho 3:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini wakati wowote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini, wakati mtu amgeukiapo Bwana, kifuniko hicho huondolewa. Biblia Habari Njema - BHND Lakini, wakati mtu amgeukiapo Bwana, kifuniko hicho huondolewa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini, wakati mtu amgeukiapo Bwana, kifuniko hicho huondolewa. Neno: Bibilia Takatifu Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana Mungu Mwenyezi, utaji unaondolewa. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana Isa, utaji unaondolewa. BIBLIA KISWAHILI Lakini wakati wowote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa. |
Lakini desturi ya Musa ilikuwa alipoingia mbele za BWANA kusema naye, kuuvua huo utaji mpaka atoke; akatoka akawaambia wana wa Israeli maneno yote aliyoambiwa.
Naye katika mlima huu atauharibu utando uliowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote.
Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho kitabu, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.
Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
Na hao pia, wasipokaa katika kutoamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena.
ukiwa utaifuata sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa kuyashika maagizo yake, na amri zake zilizoandikwa katika kitabu hiki cha torati; ukimwelekea BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote.
Na wakati uwapo katika mashaka, ukiisha kupatwa na mambo haya yote, siku za mwisho, utamrudia BWANA, Mungu wako, na kuisikiza sauti yake;