Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
2 Wakorintho 13:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini natumaini kama mtajua ya kuwa sisi hatukukataliwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini natumaini kwamba nyinyi mnajua kuwa sisi hatukushindwa. Biblia Habari Njema - BHND Lakini natumaini kwamba nyinyi mnajua kuwa sisi hatukushindwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini natumaini kwamba nyinyi mnajua kuwa sisi hatukushindwa. Neno: Bibilia Takatifu Natumaini mtaona kuwa sisi hatukushindwa. Neno: Maandiko Matakatifu Natumaini mtaona kuwa sisi hatukushindwa. BIBLIA KISWAHILI Lakini natumaini kama mtajua ya kuwa sisi hatukukataliwa. |
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong'onezo, na majivuno, na ghasia;
Kwa sababu hiyo, naandika haya nikiwa mbali nanyi, ili, nikija, nisiwe na ukali wa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.
Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.
Nasi tunamwomba Mungu, msifanye lolote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, ijapokuwa sisi tu kama waliokataliwa.