2 Wakorintho 12:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika subira yote, kwa ishara na maajabu na miujiza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Miujiza na maajabu yaoneshayo wazi kwamba mimi ni mtume yalifanyika miongoni mwenu kwa uvumilivu wote. Biblia Habari Njema - BHND Miujiza na maajabu yaoneshayo wazi kwamba mimi ni mtume yalifanyika miongoni mwenu kwa uvumilivu wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Miujiza na maajabu yaoneshayo wazi kwamba mimi ni mtume yalifanyika miongoni mwenu kwa uvumilivu wote. Neno: Bibilia Takatifu Mambo yanayomtambulisha mtume wa kweli, yaani ishara, miujiza na maajabu, yalifanywa miongoni mwenu kwa saburi nyingi. Neno: Maandiko Matakatifu Mambo yanayomtambulisha mtume wa kweli, yaani, ishara, miujiza na maajabu, yalifanywa miongoni mwenu kwa saburi nyingi. BIBLIA KISWAHILI Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika subira yote, kwa ishara na maajabu na miujiza. |
Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au Injili nyingine msiyoikubali, mnavumiliana naye punde!
Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena, hii si hali yangu katika elimu; ila katika kila neno tumedhihirishwa kwenu.
lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.