Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.
2 Wakorintho 10:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia. Biblia Habari Njema - BHND Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia. Neno: Bibilia Takatifu Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. Neno: Maandiko Matakatifu Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. BIBLIA KISWAHILI Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; |
Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.
kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyaua matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
Basi, nilipokusudia hayo, je! Nilitumia kigeugeu? Au hayo niyakusudiayo, nayakusudia kwa jinsi ya mwili kwamba iwe hivi kwangu, kusema Ndiyo, ndiyo, na Siyo, siyo?
(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyonenwa awali juu yako, ili katika hayo uweze kupigana vile vita vizuri;
Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa subira katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,