2 Wafalme 4:37 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo akaingia, akamwangukia miguu akainama mpaka nchi; kisha akamchukua mwanawe, akatoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akainama miguuni pa Elisha kwa shukrani na kumchukua mwanawe. Biblia Habari Njema - BHND Akainama miguuni pa Elisha kwa shukrani na kumchukua mwanawe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akainama miguuni pa Elisha kwa shukrani na kumchukua mwanawe. Neno: Bibilia Takatifu Akaingia ndani, akaanguka miguuni pa Al-Yasa na kusujudu hadi chini. Kisha akamchukua mwanawe na kutoka nje. Neno: Maandiko Matakatifu Akaingia ndani, akaanguka miguuni pa Al-Yasa na kusujudu hadi nchi. Kisha akamchukua mwanawe na kutoka nje. BIBLIA KISWAHILI Ndipo akaingia, akamwangukia miguuni akainama mpaka chini; kisha akamchukua mwanawe, akatoka. |
Mwanamke akamwambia Eliya, Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la BWANA kinywani mwako ni kweli.
Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.
Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.
Akamwita Gehazi, akasema, Mwite yule Mshunami. Basi akamwita. Na alipofika kwake, Elisha akasema, Haya! Mchukue mwanao.
Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;