2 Wafalme 4:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi akaingia ndani, akajifungia mlango, yeye na yule mtoto wote wawili, akamwomba BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, akafunga mlango na kumwomba Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, akafunga mlango na kumwomba Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, akafunga mlango na kumwomba Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Akaingia ndani, akajifungia yeye na yule mtoto, akamwomba Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Akaingia ndani, akajifungia yeye na yule mtoto, akamwomba bwana. BIBLIA KISWAHILI Basi akaingia ndani, akajifungia mlango, yeye na yule mtoto wote wawili, akamwomba BWANA. |
Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.
Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nilidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la BWANA, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma.
Hata walipokwisha kuingia Samaria, Elisha akasema, BWANA wafumbue macho watu hawa, wapate kuona. BWANA akawafumbua macho wakaona; kumbe! Walikuwa katikati ya Samaria.
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Alipofika nyumbani hakuruhusu mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.
Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, inuka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.