Ikawa, baada ya hayo, mwana wake yule mwanamke, bibi wa nyumba ile, akaugua; ugonjwa wake ukazidi hata akawa hana pumzi tena.
2 Wafalme 4:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Elisha alipofika nyumbani, tazama, mtoto amekwisha kufa, amelazwa kitandani pake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Elisha alipofika, akaingia peke yake chumbani na kuona maiti ya kijana kitandani. Biblia Habari Njema - BHND Elisha alipofika, akaingia peke yake chumbani na kuona maiti ya kijana kitandani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Elisha alipofika, akaingia peke yake chumbani na kuona maiti ya kijana kitandani. Neno: Bibilia Takatifu Al-Yasa alipofika kwenye ile nyumba, mtoto alikuwa amelala juu ya kitanda chake angali amekufa. Neno: Maandiko Matakatifu Al-Yasa alipofika kwenye ile nyumba, mtoto alikuwa amelala juu ya kitanda chake angali amekufa. BIBLIA KISWAHILI Basi Elisha alipofika nyumbani, tazama, mtoto amekwisha kufa, amelazwa kitandani pake. |
Ikawa, baada ya hayo, mwana wake yule mwanamke, bibi wa nyumba ile, akaugua; ugonjwa wake ukazidi hata akawa hana pumzi tena.
Mamaye akapanda juu, akamlaza juu ya kitanda cha yule mtu wa Mungu, akamfungia mlango, akatoka.
Na Gehazi akawatangulia, akaiweka ile fimbo juu ya uso wa mtoto; lakini hapakuwa na sauti, wala majibu. Basi akarudi ili kumlaki, akamwambia, akisema, Mtoto hakuamka.
Basi akaingia ndani, akajifungia mlango, yeye na yule mtoto wote wawili, akamwomba BWANA.