Yule mwanamke akachukua mimba, akazaa mtoto wa kiume wakati uo huo mwakani, kama Elisha alivyomwambia.
2 Wafalme 4:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata yule mtoto alipokua, ikawa siku moja alitoka kwenda kwa baba yake kwenye wavunao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtoto huyo alipokua, alitoka siku moja pamoja na baba yake akafuatana na wavunaji, Biblia Habari Njema - BHND Mtoto huyo alipokua, alitoka siku moja pamoja na baba yake akafuatana na wavunaji, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtoto huyo alipokua, alitoka siku moja pamoja na baba yake akafuatana na wavunaji, Neno: Bibilia Takatifu Mtoto akakua, naye siku moja akamwendea baba yake, aliyekuwa pamoja na wavunaji. Neno: Maandiko Matakatifu Mtoto akakua, naye siku moja akamwendea baba yake, ambaye alikuwa pamoja na wavunaji. BIBLIA KISWAHILI Hata yule mtoto alipokua, ikawa siku moja alitoka kwenda kwa baba yake kwa wavunao. |
Yule mwanamke akachukua mimba, akazaa mtoto wa kiume wakati uo huo mwakani, kama Elisha alivyomwambia.
Akamwambia baba yake, Kichwa changu! Kichwa changu! Naye akamwambia mtumishi wake, Mchukue kwa mama yake.
Basi Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke, ambaye alimfufulia mwanawe, akasema, Ondoka, ukaende wewe na jamaa yako, ukae hali ya kigeni utakakoweza kukaa; kwa sababu BWANA ameiita njaa; nayo itakuja juu ya nchi hii muda wa miaka saba.
Na tazama, Boazi akaja kutoka Bethlehemu na kuwaamkia wavunaji, akasema, BWANA akae nanyi. Nao wakamwitikia, BWANA na akubariki.