Wakati ule watumishi wa Nebukadneza mfalme wa Babeli wakakwea kwenda Yerusalemu, na mji ukahusuriwa.
2 Wafalme 25:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi mji huo ulihusuriwa hata mwaka wa kumi na moja wa mfalme Sedekia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mji uliendelea kuzingirwa mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia. Biblia Habari Njema - BHND Mji uliendelea kuzingirwa mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mji uliendelea kuzingirwa mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia. Neno: Bibilia Takatifu Mji ulizingirwa na jeshi hadi mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Mfalme Sedekia. Neno: Maandiko Matakatifu Mji ulizungukwa na jeshi mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Mfalme Sedekia. BIBLIA KISWAHILI Basi mji huo ulihusuriwa hata mwaka wa kumi na moja wa mfalme Sedekia. |
Wakati ule watumishi wa Nebukadneza mfalme wa Babeli wakakwea kwenda Yerusalemu, na mji ukahusuriwa.
Ikawa katika mwaka wa tisa wa kutawala kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, kupigana na Yerusalemu, akapanga hema zake kuukabili; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.
Siku ya tisa ya mwezi wa nne njaa ilikuwa nzito ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi.
Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, katika mwaka wa kumi wa Sedekia, mfalme wa Yuda, nao ulikuwa mwaka wa kumi na nane wa Nebukadneza.
Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa BWANA, Mungu wako.