Akavifanya vile vitako kumi vya shaba; mikono minne urefu wa kitako kimoja, na mikono minne upana wake, na mikono mitatu kwenda juu kwake.
2 Wafalme 25:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Zile nguzo mbili, na ile bahari moja, na vile vitako, Sulemani alivyoifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shaba yote nyeusi aliyotumia Solomoni kutengeneza zile nguzo mbili, birika lile kubwa na vikalio kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu haikuweza kupimwa kwa uzito. Biblia Habari Njema - BHND Shaba yote nyeusi aliyotumia Solomoni kutengeneza zile nguzo mbili, birika lile kubwa na vikalio kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu haikuweza kupimwa kwa uzito. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shaba yote nyeusi aliyotumia Solomoni kutengeneza zile nguzo mbili, birika lile kubwa na vikalio kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu haikuweza kupimwa kwa uzito. Neno: Bibilia Takatifu Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Sulemani alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, ilikuwa na uzito mwingi usioweza kupimika. Neno: Maandiko Matakatifu Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Sulemani alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la bwana, ilikuwa na uzito usioweza kupimika. BIBLIA KISWAHILI Zile nguzo mbili, na ile bahari moja, na vile vitako, Sulemani alivyoifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani. |
Akavifanya vile vitako kumi vya shaba; mikono minne urefu wa kitako kimoja, na mikono minne upana wake, na mikono mitatu kwenda juu kwake.
Sulemani akaviacha vyombo vyote visipimwe kwa kuwa vilikuwa vingi mno; wala uzito wa shaba haukujulikana.
Na vyetezo, na mabakuli; vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, kamanda wa askari walinzi akavichukua.
Nguzo mbili, beseni, na ng'ombe kumi na mbili za shaba zilizokuwa chini ya vikalio vyake, ambavyo mfalme Sulemani aliifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vitu hivyo vyote ilikuwa haiwezi kupimwa kwa kuwa nyingi sana.