2 Wafalme 23:37 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na yote waliyoyafanya baba zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yehoyakimu alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama waliyoyafanya babu zake wote. Biblia Habari Njema - BHND Yehoyakimu alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama waliyoyafanya babu zake wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yehoyakimu alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama waliyoyafanya babu zake wote. Neno: Bibilia Takatifu Naye akafanya maovu machoni mwa Mwenyezi Mungu, kama baba zake walivyokuwa wamefanya. Neno: Maandiko Matakatifu Naye akafanya maovu machoni mwa bwana, kama baba zake walivyokuwa wamefanya. BIBLIA KISWAHILI Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na yote waliyoyafanya baba zake. |
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja; akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Mungu wake.
Nami nitamwadhibu yeye, na wazao wake, na watumishi wake, kwa sababu ya uovu wao, nami nitaleta juu yao, na juu ya wenyeji wa Yerusalemu, na juu ya watu wa Yuda, mabaya yote niliyoyatamka juu yao, lakini hawakukubali kusikiliza.