Kwa sababu Manase mfalme wa Yuda amefanya machukizo haya, na kutenda vibaya kuliko yote waliyoyatenda Waamori, waliokuwa kabla yake, naye akawakosesha Yuda kwa sanamu zake;
2 Wafalme 21:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akaiendea njia yote aliyoiendea baba yake, akazitumikia sanamu alizozitumikia baba yake, akaziabudu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alifuata njia yote aliyoiendea baba yake na kutumikia sanamu ambazo baba yake alizitumikia na kuziabudu. Biblia Habari Njema - BHND Alifuata njia yote aliyoiendea baba yake na kutumikia sanamu ambazo baba yake alizitumikia na kuziabudu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alifuata njia yote aliyoiendea baba yake na kutumikia sanamu ambazo baba yake alizitumikia na kuziabudu. Neno: Bibilia Takatifu Akaenenda katika njia zote za baba yake, akaabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu na kuzisujudia. Neno: Maandiko Matakatifu Akaenenda katika njia zote za baba yake, akaabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu na kuzisujudia. BIBLIA KISWAHILI Akaiendea njia yote aliyoiendea baba yake, akazitumikia sanamu alizozitumikia baba yake, akaziabudu. |
Kwa sababu Manase mfalme wa Yuda amefanya machukizo haya, na kutenda vibaya kuliko yote waliyoyatenda Waamori, waliokuwa kabla yake, naye akawakosesha Yuda kwa sanamu zake;
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.
Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya BWANA, mfalme akazivunja, akaziteremsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.
Tena wenye pepo wa utambuzi, na wachawi, na vinyago, na sanamu, na machukizo yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, Yosia akayaondoa yote, ili apate kuyathibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya BWANA.