BWANA asema hivi, Tazama, mimi nitaleta uovu juu ya mahali hapa, na juu yao wakaao hapa, naam, maneno yote ya kitabu alichokisoma mfalme wa Yuda;
2 Wafalme 21:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalia, naleta mabaya juu ya Yerusalemu na juu ya Yuda, hata kila mtu asikiaye, masikio yake yatawasha yote mawili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema basi, sasa, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, tazama nitaleta juu ya Yerusalemu na Yuda, msiba ambao hata yeyote atakayesikia atashtuka. Biblia Habari Njema - BHND basi, sasa, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, tazama nitaleta juu ya Yerusalemu na Yuda, msiba ambao hata yeyote atakayesikia atashtuka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza basi, sasa, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, tazama nitaleta juu ya Yerusalemu na Yuda, msiba ambao hata yeyote atakayesikia atashtuka. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Nitaleta maafa makubwa juu ya Yerusalemu na Yuda, kiasi kwamba masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yatawasha. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo hili ndilo asemalo bwana, Mungu wa Israeli: Nitaleta maafa makubwa juu ya Yerusalemu na Yuda, kiasi kwamba masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yatawasha. BIBLIA KISWAHILI kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalia, naleta mabaya juu ya Yerusalemu na juu ya Yuda, hata kila mtu asikiaye, masikio yake yatawasha yote mawili. |
BWANA asema hivi, Tazama, mimi nitaleta uovu juu ya mahali hapa, na juu yao wakaao hapa, naam, maneno yote ya kitabu alichokisoma mfalme wa Yuda;
Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.
kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.
ukisema, Lisikieni neno la BWANA, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu yeyote akisikia habari yake, masikio yake yatawasha.
Bwana MUNGU asema hivi; Ni jambo baya, jambo baya la namna ya peke yake; angalia, linakuja.
Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.
Ni ninyi tu niliowajua katika jamaa zote zilizo duniani; kwa sababu hiyo nitawapatiliza ninyi maovu yenu yote.
Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.
BWANA akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha.