Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno yote ya kamanda huyu, ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; naye atayakemea hayo maneno aliyoyasikia BWANA, Mungu wako; kwa sababu hii inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.
Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; BWANA asema hivi, Usiyaogope maneno hayo uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.
Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; BWANA asema hivi, Usiyaogope maneno uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.