2 Wafalme 19:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Hukusikia wewe ya kuwa mimi ndimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale? Sasa mimi nimelitimiza jambo hili, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, hata ikawe chungu na magofu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ‘Je, hujasikia, kwamba nilipanga jambo hili tangu awali? Ninachotekeleza sasa nilikipanga zamani.’ Nilikuweka uijenge miji yenye ngome kwa rundo la magofu. Biblia Habari Njema - BHND ‘Je, hujasikia, kwamba nilipanga jambo hili tangu awali? Ninachotekeleza sasa nilikipanga zamani.’ Nilikuweka uijenge miji yenye ngome kwa rundo la magofu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ‘Je, hujasikia, kwamba nilipanga jambo hili tangu awali? Ninachotekeleza sasa nilikipanga zamani.’ Nilikuweka uijenge miji yenye ngome kwa rundo la magofu. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Je, hujasikia? Zamani sana niliamuru hili. Siku za kale nilipanga hili; sasa nimelifanya litokee, kwamba umegeuza miji yenye ngome kuwa malundo ya mawe. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Je, hujasikia? Zamani sana niliamuru hili. Siku za kale nilipanga hili; sasa nimelifanya litokee, kwamba umegeuza miji yenye ngome kuwa malundo ya mawe. BIBLIA KISWAHILI Je! Hukusikia wewe ya kuwa mimi ndimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale? Sasa mimi nimelitimiza jambo hili, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, hata ikawe chungu na magofu. |
Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.
Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.
Dondokeni, enyi mbingu, toka juu, Mawingu na yamwage haki; Nchi na ifunuke, ili kutoa wokovu, Nayo itoe haki ikamee pamoja; Mimi, BWANA, nimeiumba.
Tazama, nimemwumba mhunzi afukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu.
Kwa ajili ya hayo nitafanya Samaria kuwa kama chungu katika shamba, na kama miche ya shamba la mizabibu; nami nitayatupa mawe yake bondeni, nami nitaifunua misingi yake.