Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

2 Wafalme 16:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Ahazi akatwaa fedha na dhahabu iliyoonekana katika nyumba ya BWANA, na katika hazina za nyumba ya mfalme, akazipeleka kwa mfalme wa Ashuru kuwa zawadi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ahazi akachukua fedha na dhahabu iliyokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na hazina iliyokuwa katika nyumba ya mfalme na kumpelekea kama zawadi mfalme wa Ashuru.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ahazi akachukua fedha na dhahabu iliyokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na hazina iliyokuwa katika nyumba ya mfalme na kumpelekea kama zawadi mfalme wa Ashuru.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ahazi akachukua fedha na dhahabu iliyokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na hazina iliyokuwa katika nyumba ya mfalme na kumpelekea kama zawadi mfalme wa Ashuru.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Naye Ahazi akachukua fedha na dhahabu zilizopatikana ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na katika hazina ya jumba la mfalme, na kuzituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Naye Ahazi akachukua fedha na dhahabu zilizopatikana ndani ya Hekalu la bwana na katika hazina ya jumba la mfalme, na kuzituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ahazi akatwaa fedha na dhahabu iliyoonekana katika nyumba ya BWANA, na katika hazina za nyumba ya mfalme, akazipeleka kwa mfalme wa Ashuru kuwa zawadi.

Tazama sura
Tafsiri zingine

2 Wafalme 16:8
13 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mambo yote ya Yoashi yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?

Akaja Pulu mfalme wa Ashuru juu ya nchi; naye Menahemu akampa Pulu talanta elfu moja za fedha, ili kwamba mkono wake uwe pamoja naye, na ufalme uwe imara mkononi mwake.

Naye Shalmanesa mfalme wa Ashuru akakwea juu yake, Hoshea akawa mtumishi wake, akampa kodi.

Ndipo Asa akatoa fedha na dhahabu katika hazina za nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, akampelekea Ben-hadadi mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema,

Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapeana mikono na wana wa wageni.

BWANA ataleta juu yako, na juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako, siku zisizokuja bado, tangu siku ile aliyoondoka Efraimu kutoka katika Yuda; yaani, mfalme wa Ashuru.

Kwa hiyo mtaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia; Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.