Naye Uria kuhani akajenga madhabahu; sawasawa na yote aliyomletea mfalme Ahazi kutoka Dameski; ndivyo alivyoifanya Uria kuhani iwe tayari atakaporudi mfalme Ahazi kutoka Dameski.
2 Wafalme 16:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akafanya hivyo Uria kuhani, sawasawa na yote aliyoyaamuru mfalme Ahazi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Uria akafuata maagizo ya mfalme. Biblia Habari Njema - BHND Naye Uria akafuata maagizo ya mfalme. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Uria akafuata maagizo ya mfalme. Neno: Bibilia Takatifu Naye Uria kuhani akafanya kama Mfalme Ahazi alivyoagiza. Neno: Maandiko Matakatifu Naye Uria kuhani akafanya kama Mfalme Ahazi alivyoagiza. BIBLIA KISWAHILI Akafanya hivyo Uria kuhani, sawasawa na yote aliyoyaamuru mfalme Ahazi. |
Naye Uria kuhani akajenga madhabahu; sawasawa na yote aliyomletea mfalme Ahazi kutoka Dameski; ndivyo alivyoifanya Uria kuhani iwe tayari atakaporudi mfalme Ahazi kutoka Dameski.
Mfalme Ahazi akamwamuru Uria kuhani, akisema, Juu ya madhabahu hiyo kubwa uiteketeze sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, na sadaka ya unga ya jioni, na sadaka ya mfalme ya kuteketezwa, na sadaka yake ya unga, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya watu wote wa nchi, na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji; ukanyunyize juu yake damu yote ya sadaka ya kuteketezwa, na damu yote ya dhabihu; bali madhabahu ya shaba itakuwa kwangu mimi ili niiulizie.
Mfalme Ahazi akakata papi za vitako, akaliondoa lile birika juu yake; akaiteremsha ile bahari itoke juu ya ng'ombe za shaba zilizokuwa chini yake, akaiweka juu ya sakafu ya mawe.
Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya BWANA, napo ndipo alipopanena BWANA, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu.
Akajenga madhabahu katika nyumba ya BWANA, pale ndipo alipopanena BWANA, Katika Yerusalemu litakuwako jina langu milele.
nami nitajipatia mashahidi waaminifu ili kuandika habari, yaani, Uria, kuhani, na Zekaria, mwana wa Yeberekia.
Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa BWANA wa majeshi.
Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kama ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.
Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya malipo, nao wameangamia katika maasi ya Kora.