makuhani na waitwae, kila mtu kwa hao awajuao; nao watatengeneza palipobomoka nyumbani, kila mahali palipoonekana pamebomoka.
2 Wafalme 12:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini ikawa, mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani walikuwa hawajatengeneza mabomoko ya nyumba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini hata baada ya miaka ishirini na mitatu ya mfalme Yoashi makuhani walikuwa bado hawajafanya marekebisho yoyote ya nyumba. Biblia Habari Njema - BHND Lakini hata baada ya miaka ishirini na mitatu ya mfalme Yoashi makuhani walikuwa bado hawajafanya marekebisho yoyote ya nyumba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini hata baada ya miaka ishirini na mitatu ya mfalme Yoashi makuhani walikuwa bado hawajafanya marekebisho yoyote ya nyumba. Neno: Bibilia Takatifu Lakini ikawa kufikia mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake Mfalme Yoashi, makuhani walikuwa bado hawajalikarabati Hekalu. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini ikawa kufikia mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake Mfalme Yoashi, makuhani walikuwa bado hawajalikarabati Hekalu. BIBLIA KISWAHILI Lakini ikawa, mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani walikuwa hawajafanya matengenezo ya nyumba. |
makuhani na waitwae, kila mtu kwa hao awajuao; nao watatengeneza palipobomoka nyumbani, kila mahali palipoonekana pamebomoka.
Ndipo mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani, na makuhani wengine, akawauliza, Mbona hamtengenezi mabomoko ya nyumba? Basi sasa msipokee tena fedha kwa hao mwajuao, lakini itoeni kwa ajili ya mabomoko ya nyumba.
Akawakusanya makuhani na Walawi, akawaambia, Nendeni katika miji ya Yuda, mkakusanye fedha kutoka Israeli wote, ili kuitengeneza nyumba ya Mungu wenu mwaka kwa mwaka, mkafanye bidii kuliharakisha neno hili. Lakini Walawi hawakuliharakisha.
Lakini makuhani walikuwa wachache, wasiweze kuchuna sadaka zote za kuteketezwa; basi ndugu zao Walawi wakawasaidia, hadi kazi ilipokwisha na hadi makuhani walipojitakasa; kwa kuwa Walawi walikuwa wenye mioyo ya adili kwa kujitakasa kuliko makuhani.
Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.
lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.