wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na kikomo, zinazozua maswali wala si mpango wa Mungu ulio katika imani; basi uwaambie hivyo.
2 Timotheo 2:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi. Biblia Habari Njema - BHND Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi. Neno: Bibilia Takatifu Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa unajua hayo huzaa magomvi. Neno: Maandiko Matakatifu Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa wajua ya kwamba hayo huzaa magomvi. BIBLIA KISWAHILI Lakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo ya elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi. |
wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na kikomo, zinazozua maswali wala si mpango wa Mungu ulio katika imani; basi uwaambie hivyo.
Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wanaoyasikia.
Jiepushe na maneno machafu yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,
Lakini ujiepushe na mabishano ya kipumbavu, nasaba, magomvi, na mabishano ya sheria. Kwa kuwa hayana manufaa, tena hayafai kitu.
Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?